12 Aprili 2015 - 18:19
 Hillary Clinton atangaza rasmi kugombea Urais Marekani

Hillary Rodham Clinton mke wa Rais wa zamani wa Marekani na ambaye pia aliwahi kuwa waziri wa mambo ya nje anatarajiwa kutangaza rasmi hii leo azma yake ya kugombea urais kupitia tiketi ya chama tawala cha Democrats katika uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Hillary Rodham Clinton mke wa Rais wa zamani wa Marekani na ambaye pia aliwahi kuwa waziri wa mambo ya nje anatarajiwa kutangaza rasmi hii leo azma yake ya kugombea urais kupitia tiketi ya chama tawala cha Democrats katika uchaguzi mkuu mwaka ujao. Azma hiyo imepata nguvu hapo jana baada ya Rais wa Marekani Barack Obama kusema atakuwa Rais stadi. Hii itakuwa mara ya pili kwa Bi Clinton kuwania urais baada ya kushindwa na Obama katika uchaguzi wa uteuzi wa mgombea wa vyama mwaka 2008.

Duru zinaarifu kuwa Bi Clinton mwenye umri wa miaka 67 atatangaza nia yake ya kutaka kuwa Rais wa Marekani kupitia mitandao ya kijamii kabla ya kusafiri wiki ijayo kuelekea jimbo la Iowa ambako vyama vikuu vya kisiasa vitawachagua wagombea wao wa urais.Wanasiasa wawili wa chama cha Republican Ted Cruz na Rand Paul wameshatangaza rasmi nia yao ya kugombea Urais.